Mambo 10 Usiyoyajua Kumhusu Bruce Lee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wapenzi wengi wa filamu wanamtambua na kumuenzi sana marehemu mwigizaji Bruce Lee kutokana na weledi wake kwenye filamu na sanaa ya Kung Fu zilizowazingua wengi kwenye taaluma yake ya uigizaji. Bruce Lee (1940 - 1973) aliyejulikana kwa majina kamili kama Lee Jun-fan alisifika sana kwa kubuni mtindo wa kupigana kwa Kungfu kwa jina ‘Jeet Kune Do’ na kuigiza filamu nyingi.

Kando na kuwa alipenda sama mchezo wa ndondi, kuna mambo mengi ya kushangaza ambayo yalizingira maisha ya Bruce Lee wakati wa taaluma yake ya uigizaji na karate ambazo zitakushangaza.

1. Bruce Lee alifanya mazoezi kwa makonde 5,000 kila siku ili kuwa na ujuzi wa juu zaidi katika kupigana. Alikuwa na bidii na hilo linaeleza kwa nini makonde yake yalikuwa mazito kwa wapinzani wake kwenye filamu na mapigano. 2. Bruce Lee alikuwa akiitoboa mikebe kwa vidole vyake. Siku za zamani, mikebe haikutengenezwa kwa mabati nyepesi, lakini aliweza kuvifungua kwa vidole vyake. Aliwahi kujeruhiwa kwenye vidole vyake alipokuwa akionyesha ujuzi wake kwenye maonyesho ya ‘Big Boss’ na hiyo ndiyo sababu alifunga vidole vyake kwa bandeji kwenye filamu nyingi alizoigiza. 3. Bruce Lee alikuwa na kasi ya aina yake. Alionyesha kasi yake kwa kuweka sarafu mikononi mwa mtu na kuichukua kabla ya mtu huyo kuifunika kiganjani ili kumzuia kuitwaa.

4. Viungo vya kutoa jasho kwenye makwapa vya Bruce Lee viliondolewa kwa upasuaji mwaka wa 1972.

Alisemekana kukerwa na kutokwa kwa jasho jingi kwenye makwapa na jinsi jasho hiyo ilivyoonekana vibaya, hali iliyomfanya kufanyiwa upasuaji huo.

Sijui jinsi upasuaji wa aina hiyo unavyoweza kufanyika.

5. Akiwa mvulana barobaro, Bruce Lee alikuwa mtoto nyota wa uigizaji huko Hong Kong.

Alikuwa ameigiza filamu 20 alipokuwa na miaka 18.

6. Bruce Lee aliandika mashairi mengi ambayo zilijumuishwa kwenye kitabu chake ‘The Tao of Jeet Kune Do’.

Marafiriki zake waliarifu kuwa alipenda sana kuandika mashairi kila mara. Waliomuita msanii hawakukosea.

7. Bruce Lee alitembea na bunduki aina ya 357 Magnum. Hilo lilikuwa kwa sababu ya usalama wake kwa kuwa ikiwa kila mtu alitaka kupigana naye ili kudhihirisha ubabe wao, basi alihofia maisha yake kama mtu yeyote yule.

Jesse Glover alidhibitisha kuwa alikuwa na ujuzi mkubwa na uhakika wa kipekee wa kufyatua risasi kwa kutumia bunduki.

8. Kifo cha Bruce Lee bado kinaaminika kuwa cha kutatanisha. Madai mengi yaliibuka zikiwemo kutumia bangi kama ilivyodhaniwa na baadhi ya madaktari wake, kuuawa kwa sumu ambapo watu wengine waliamini kuwa Raymond Chow alitaka auawe.

Chanzo cha kifo chake bado kinajadiliwa na jamaa, marafiki na mashabiki wake.

9. Bruce alipenda kusoma sana na kupekua vitabu kutoka kwenye jalada hadi ukurasa wa mwisho.

Alikuwa na maktaba ya zaidi ya vitabu 2,000.

Alijulikana kwa kusoma kitabu, kutazama runinga na kuinua kifaa cha uzito cha kufanya mazoezi kwa wakati mmoja!

10. Bruce Lee hangeweza kuogelea.

Kakake mdogo, Robert na dadake, Phoebe walifichua kuwa Bruce alichukia maji na hangeweza kuogelea.
Ufichuzi huo ulidhibitisha udhaifu wake mkubwa uliohusiana na maji.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad