7/17/2020

Ni ‘Impossible’ Kupata Mbadala wa Pogba, Rio Ferdinand Awaonya Man United Mchana KweupeAliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand amemsisitiza kocha Ole Gunnar Solskjaer kuwa lazima ahakikishe anambakiza kiungo wake Paul Pogba kipindi hiki cha majira ya joto kwa kuwa kupata mbadala wake ndani ya Old Trafford ni kitu kisichowezekana kabisa.Mfaransa huyo Paul Pogba ambaye pia ni mshindi wa taji la kombe la Dunia mara kadhaa aliwahi kusikika akitangaza kutaka kuondoka United ili kwenda kupata changamoto mahali pengine wakati msimu huu wa 2019/20 ukielekea mwishoni.

Kiungo huyo mara kadhaa amekuwa akisumbuliwa na majeraha kabla ya kuibuka kwa janga la corona uliyopelekea kuwekwa kwa ‘lockdown,’ huku akiwa mekosekana katika michezo nane chini Solskjaer.

Lakini nyota huyo wazamani wa Juventus amekuwa kivutio kikubwa uwanjani tangu kuanza upya kwa msimu baada ya Corona, akifanikiwa kucheza kwenye ushindi wao dhidi ya Crystal Palace.

Ferdinand ameutaka uongozi wa United kuhakikisha Pogba wana muongezea mkataba baada ya huu wa sasa kukfikia tamati mwaka 2021.“Kwa sasa yupo kwenye kiwango chake. Kwa nini mtake kumuuza sasa ?, hivi ni nani huyo bora mwenye kiwango cha dunia mtakaye mnunua na kumleta kwa sasa, ni kitu kischowezekana kupata mbadala wake.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger