7/29/2020

"Nimeitwa Tasa, Mgumba Lakini Nimezaa" - Wanjara


Miss Mara, Mwanamitindo na aliyewahi kuwa mpenzi wa zamani wa Prof Jay, Rashida Wanjara amesema anajisikia furaha kuwa mzazi kama wazazi wengine baada ya watu kumsema sana kwamba yeye ni tasa na mgumba kwamba hataweza kupata watoto.


Rashida Wanjara amesema wakati wa Mungu ni wakati sahihi ila ujana na maamuzi ndiyo ulimchelewesha asipate mtoto japo watu walidhani kwamba hataweza kupata mtoto.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Rashida Wanjara amesema "Wakati wa Mungu ni wakati sahihi, binafsi ujana na maamuzi ndiyo vilinichelewesha kupata, wapo watu walijua kuchelewa kwangu kuzaa kwamba nina matatizo maana nimeitwa Tasa nimeitwa Mgumba, kila mtu alikuwa ananijaji anavyojua yeye ila mwisho wa siku ukweli nilikuwa naujua mimi mwenyewe"

Aidha Rashida Wanjara ameongeza kusema amepata mtoto wa kiume, jina lake ni Shayan ambalo asili yake ni uarabuni na maana yake ni mtu tajiri
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger