7/17/2020

"Ukikosa Rafiki Mbunge Mwaka Huu, Hupati Tena"


Mchakato wa kutafuta Wabunge mwaka huu 2020 umechangamka sana, kwa sababu watu tofauti tofauti na sura mpya zimejitokeza kuchukua fomu ya kugombania majimbo mbalimbali, ambapo unaweza kutumia msemo wa kwamba "ukikosa rafiki Mbunge mwaka huu, hupati tena".


Producer Mkongwe Master J ambaye ametia nia ya kuwania Ubunge Rombo, Kilimanjaro kupitia chama cha CCM

Tukiangalia kwenye tasnia ya burudani tayari wasanii na watu maarufu, wameshachukua fomu ya kugombea Ubunge kwenye majimbo yao husika kwa mfano.

Master J - Producer huyu ni mkongwe wa muziki wa BongoFleva, amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro kupitia CCM.

Wakazi, ambaye jina lake kamili ni Webiro Wasira, tayari amechukua fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Ukonga, kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Bonta Maarifa, kutoka kampuni ya Weusi na amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini kupitia CCM.

Lilian Kamazima ambaye alikuwa ni Miss Tanzania mwaka 2014, yupo kwenye orodha ya watia nia ya kuutaka Ubunge na tayari amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalum kupitia CCM Mkoa wa Arusha.

MC Pilipili, amabaye ni mshehereshaji na mchekeshaji, amechukua fomu ya kuwania Ubunge kwenye Jimbo la Bahi nyumbani kwao Dodoma kupitia tiketi ya CCM.

Steve Nyerere, mapema kabisa alianza kutangaza kwamba atawania Ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini na tayari ameshafanikiwa kwenda huko na kuchukua fomu kupitia chama cha CCM.

Askofu Gwajima naye amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya chama cha CCM.

Mchopanga ambaye ni msanii wa filamu, amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Ubungo kupitia chama cha CCM.

Dr Cheni, staa wa zamani wa filamu Bongo na yeye tayari ameshachukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Ilala kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wasanii wengine ambao walitangaza watagombea Ubunge mwaka huu 2020 ila bado hawajachukua fomu ni Baba Levo (Kigoma Mjini - ACT Wazalendo) , (Shilole - Igunga, Tabora) na Mwana Fa (Muheza,Tanga).
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger