Wengine wanasema Nassari anautaka Ubunge, sijaja CCM kutangaza nia- Nassari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Joshua Nassari aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa ticket ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo July 8 2020 kwenye ukumbi wa CCM Arusha ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo hizi hapa chini ni kauli zake saba miongoni mwa mengi aliyoyazungumza ambayo unaweza kuyatazama zaidi kwenye video mwishoni mwa hizi kauli. 

“Wengine wanasema Nassari anautaka Ubunge, niwaambie sijatangaza nia mahali popote na sijaja CCM kutangaza nia, nimetafakari na pia Jamii, Wazee wa Meru na Marafiki waliofanya nikawa Mbunge mdogo kuliko wote Nchi hii wameniambia, naona CCM huku kunafaa” 

“Haikuwa kazi rahisi kufanya haya maamuzi ya kuja CCM, yale yote mnayotaka kuyasikia na kuyaona kutoka kwangu mtayasikia na kuyaona hata kama sio leo, sababu kubwa iliyonileta CCM ni kwakuwa naipenda Nchi yangu” 

“Ukiongea habari ya Ndege.. Wapingaji wanasema nani anapanda? mbona wakati wa Mwl. Nyerere hamkusema Mwl. unatupa Ndege hatuna hela ya kupanda, leo tuna Ndege 11, ile moja ni USD Mil 31, nimeingia Bungeni hatuna hata Ndege, unaachaje kumuunga mkono JPM!?” 

“Nimeamua kuiweka Nchi yangu mbele, najua wapo watakaonitukana watakaosema hili na lile kisa mimi kuhamia CCM lakini sitojali, nawashukuru Watu wa Meru kwa kuniamini kwa mihula miwili mfululizo nikiwa Mbunge mdogo kuliko wote Tanzania” 

“Watanzania wanaokwazwa kwa kuona nimeingia CCM ambao walitamani kuendelea kuniona upinzani naomba mnisamehe, siwezi kuendelea kuwa mnafiki roho yangu imekataa, sijatangaza nia na huenda nisichukue fomu, mkisema tunataka tukupe sehemu hayo tutaongea baadaye” 

“Yako mengi tutayazungumza huko mbele, nilichagua kuingia kwenye siasa ili kuijenga Nchi ndio maana nilichimba visima, nilinunua vitanda Hospitali, sasa yote ambayo nilikuwa napigania JPM ameyafanya nikimpinga nitaonekana sina akili” 

“Siku zote nafanya siasa za kiungwana, nimeshawaandikia barua CHADEMA na kiukweli naishukuru CHADEMA ilinichukua nikiwa mdogo wakanisikiliza wakaona kuna potential ndani yangu, nawashukuru kwa kunilea nitakuwa mjinga kama sitoikumbuka historia”

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uamuzi wako ni wa Busara.
    Nasikia Godillesi anamtafuta Polepole,
    mwambie ajitathmii kwannza na Ajielewe

    Saccozi ina Matatizo kuzidi shingoni.
    Takukuru wanaedelea na kazi yao.
    Faru Joni anaendeleza mtafaruku.
    Bebi anaendelea Kujibebisha.

    Yuko hoi Bin Taabani.

    ReplyDelete

Top Post Ad