8/28/2020

Aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita aachiliwa huru na Wanajeshi WalioasiAliye kuwa rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, aliyekamatwa Agosti 18 na kundi la wanajeshi lililofanya mapinduzi, ameachiliwa huru jana Alhamisi, jeshi limetangaza.  


Duru za kuaminika zinabaini kwamba mwanae, Karim Keita, alifaulu kuondoka nchini na kwa sasa yuko ukimbizini nje ya nchi.


Baraza kuu la kitaifa, lililoowekwa na wanajeshi kuiongoza nchi, "linaarifu wananchi wa Mali na jumuiya ya kimataifa kwamba aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta ameachiliwa huru na kwa sasa yuko nyumbani kwake", CNSP imetangaza kwenye mtandao wa Facebook.


Aliye kuwa rais wa Mali yuko huru na anaweza kufanya shughuli zake na kutembea anapotaka. Kwa sasayuko nyumbani kwake kwa mujibu wa afisa mmoja wa kundi hilo la wanajeshi.


Mmoja kati ya ndugu zake, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema IBK alirejea nyumbani kwake katika eneo la Sebenikoro wakati wa usiku. HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger