8/07/2020

Azam Rasmi Yamruhusu Sure Boy Kutua YangaRASMI uongozi wa Azam FC umekubali kumruhusu kiungo wao mkongwe fundi, Salum Abubakary ‘Sure Boy’ kujiunga na Yanga kwenye msimu ujao baada ya yeye mwenyewe kuonyesha nia ya kutua Jangwani.

Hiyo ikiwa siku chache tangu ziwepo taarifa za Yanga kumuwania kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kuchezesha timu na kupiga pasi safi zilizonyooka kwenda kwa wachezaji wenzake, lakini hilo litatimia ikiwa Yanga wataafikiana na wao Azam FC.

Kiungo huyo imeelezwa tayari ameufuata uongozi wa Azam FC na kuomba umruhusu aondoke hapo kwenda kutafuta changamoto nyingine ya ushindani kwingine.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria alisema kuwa hawataki kumnyima furaha kiungo huyo baada ya kuomba kuondoka na badala yake watamruhusu na kwenda kwenye hiyo timu anayoitaka.


Thabiti alisema kuwa Sure Boy ameitumikia kwa muda mrefu na mafanikio makubwa, hivyo ni wakati wa yeye sasa hivi kuondoka na kikubwa watakachokifanya kama viongozi ni kumuachia aondoke zake.

Aliongeza kuwa wanaheshimu maamuzi ya mchezaji na Azam ni sehemu kubwa ya familia yake kutokana na kipindi kirefu alichokitumikia tangu timu hiyo inapanda kucheza Ligi Kuu Bara.


“Yeye mwenyewe mchezaji aliufuata uongozi wa Azam na kuomba haende sehemu nyingine kwenda kutafuta changamoto, hivyo uongozi ukakubali kumuachia na siyo vibaya kumruhusu kwenda sehemu ambayo anaamini itampa furaha.

“Wakati Sure Boy akiomba kuondoka, juzi tulipokea barua kutoka Yanga ikimuomba Sure Boy kwenda kuitumikia timu hiyo,” alisema Zakaria.

Pamoja na hivyo taarifa zaidi kutoka Azam zilieleza kuwa uongozi unasubiri Yanga upeleke ofa rasmi ya kumnunua Sure Boy ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja, na wakiafikiana atakuwa mali ya Yanga.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger