8/12/2020

Azam waitaka Yanga Kuwaomba Radhi Juu ya Sure Boy



Uongozi wa Azam FC imesikitishwa sana na tabia ya Klabu ya Yanga ambayo waliyoifanya jana ya kumuandikia barua mchezaji wa Klabu hiyo Salum Abubakar ''Sure boy'' ya kuomba kuondoka ndani ya Klabu hiyo .
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Azam Fc, Zacharia Thabit akiwa katika Studio za East Africa Radio akidadavua jambo kuihusu Timu yake.


Akizungumza na East Africa Radio ,Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilioano wa Klabu hiyo,Zacharia Thabit ''Zaka Zakazi ''amesema kuwa barua hiyo iliyowasilishwa jana ina makosa mengi kwani imewasilishwa na mtu wa Yanga ambaye alikuwa anapeleka barua za ofa za kumtaka Sure boy mwanzoni na imeandikwa tarehe 12/08/2020 ikiwa jana ni tarehe 11/08/2020.


Zaka amesema Klabu ya Yanga imetengeneza Barua ya Salum Abubakar na pia wamefanya mazungumzo na mchezaji ambaye ana mkataba huku akidai Klabu ya Yanga haipaswi kuongea na mchezaji ambaye ana mkataba hivyo Yanga wamefanya makosa.


Hivyo Azam imeitaka klabu ya Yanga itoke hadharani na kuiomba radhi klabu ya Azam haraka iwezekanavyo kwa ilichokifanya kwani mchezaji wao (Sure boy) ameikana barua hiyo
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger