Discipline: Somo Zuri Kutoka Kwa Marehemu Bruce Lee..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Jina Bruce Lee sidhani kama ni jina ngeni kwa mtu yoyote mwenye umri kuanzia miaka 100 mpaka 10, hivyo haiana haja kumzungumzia kua ni nani hasa.! Bruce alikua mwalimu wa kung fu na mgunduzi wa staili za Jet kune-do, muigizaji na mwanafalsafa..Ni moja kati ya binaadamu wachache ambao wameweka rekodi ambazo hazitokuja kuvunjwa baadhi yao ni Leonard Da'Vinci,Yesu wa Nazareth,Genghis khan,Michael Jackson Newton, Paulo wa Tarso (mtume) n.k n.k

Bruce katika maisha yake ya miaka 32 tu aliyoishi hapa Duniani kaacha historia mbalimbali ambayo sidhani kama kuna mtu wa karne hii ya 21 anaweza kuja kuivunja, baadhi ya rekodi alizoaacha amabazo hakuna aatakaye zivunja ni kama vile...

●Bruce lee alikuwa anaweza kupiga ngumi karatasi ambazo zinaninginia hewani akazitoboa (Mimi na wewe tukipiga ngumi karatasi tutaichana sio kuitoboa)

⦁ ●Alikuwa na speed kubwa ambapo kipindi anacheza muvi zake walikua wanaweka slow motion ili kuweza kuona apigo yake, inasemekana yeye ndie binaadamu pekee aliyekuwa na spidi kali zaidi kwenye kurusha mateke na ngumi.

⦁ ●Ndani ya sekunde moja alikuwa anaweza kurusha mateke sita.

⦁ Alikuwa anaweza kupiga push-up 1500 kwa mikono miwili bila kupumzika, Push up 400 kwa mkono mmoja, alikuwa anaweza kupiga push up 200 kwa vidole viwili (Mimi sizidi 40 kwa mikono miwili)

Hizo ni baadhi ya rekodi ambazo kaacha Marehemu Bruce tujiulize Bruce alikua anafanya vipi hadi kuweza kuacha alama hizo duniani, pia akaweza kumtengeneza mwanae Brandon nae kiasi chake akafanya makubwa , lengo kuu la kuleta mada hii nimetaka tushee baadhi ya vitu ambavyo alikua anafanya hadi kuweza kufikia kuacha rekodi hizo ambazo zinaishi.

Ukimchunguza Bruce Lee utangundua alikua anatembea na vitu viwili vikuu ambavyo vilimuwezesha kufanikiwa kuacha alama duniani.

1. Bruce alikuwa Integrity Person (Mtu mwadilifu) alihakikisha anafanya kile ananchokifanya kama jinsi kinavyotakiwa kufanyika..kwa kujituma na kwa moyo wake wote.

2. Bruce alikuwa Disciplined Person (Mtu mwenye Nidhamu) alikuwa ana nidhamu ya hali ya juu hasa kwa kile anachokifanya.

Basi lengo la mada yangu ni kuangalia jinsi Nidhamu katika vile vitu tunavyofanya yaweza kutufikisha katika hatua ya kutimiza malengo mbalimbali ambayo tumejiwekea. Bruce alikua na nidhamu katika mchezo wa ngumi ndio maana kafanikiwa kutengeneza historia na rekodi hizi ambazo leo hii twazisoma. Ili kutimiza malengo yake aliweza kutengeneza Formula yake akawa anaiheshimu na kuifuata wote yaweza kutusaidia katika kufanikisha kufikia vile vitu ambavyo tunatamani kuvifikia maishani (Malengo)....Tuipitie.

⦁ ●Je wewe ni Mwanfunzi/ Kuna kitu unajifunza? Kama jibu ni Ndio basi nenda kafanye mazoezi juu ya kitu hicho (kajisomee)...kama jibu ni Hapana basi tafuta kitu ambacho hukiwezi na unapenda kujifunza kisha kakifanyie mazoezi/Kajisome.

⦁ ●Je katika taaluma yako kuna mtu ni bora zaidi yako? Kama jibu ni Ndio basi Endelea kujifunzana kufanya mazoezi... Kama jibu ni Hapana basi nenda katafute mtu ambae ni bora zaidi katika taaluma yako jilinganishe nae kisha kafanye mazoezi/kajifunze zaidi

⦁ ●Je umemaliza kujifunza/kufanya mazoezi? Kama jibu ni Ndio basi nenda kalale upumzike, kisha amka endelea kufanya mazoezi /kujifunza...Kama jibu ni Hapana basi Endelea kufanya mazoezi.

⦁ ●Je Uko unafanya mazoezi/unajifunza muda huu?
Kama jibu ni Ndio basi endelea kujifunza kila kitu kilichoko mbele yako na kamwe usiache kujifunza vitu Vipya.

Hizo hapo juu ni kanuni alizo jiwekea Bruce lee ili kuweza kutimiza malengo yake, hivyo basi kama utaona yanafaa ili kutimiza malengo yako basi yafuate. kama unagonga Code ndelea kujifunza na kufanya mazoezi siku moja utatoboa, kama ni mtu Mechanical endelea kujifunza na kufanya mazoezi siku moja utatengeneza gari lako, kama unataka kuplan Heist (Wizi wa kutumia akili) endelea kujifunza jinsi ya kufanikisha tukio lako siku moja utafanikisha, Kama unatamani siku moja uje kua mwanasiasa na mwandiplomasia bora endelea kujifunza siku moja utaacha historia nzuri kwenye taifa lako...Nidhamu ndio kila kitu katika kufanya kitu ulichokusudia,heshimu unachofanya na ukipendehata kama watu wengine wanakubeza "I assure you brother one Day sun will shine to You" Brothers n Sisters hatukuumbwa kushindwa, mafanikio ndio hatima tuliyopewa ila tutayapata pale tu tutakapo weka nidhamu kwa yale tuyafanyayo. Never Give up! Never stop Learning, Dont Never in anything.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad