4/19/2022

HII Ndiyo DNA ya Kitamaduni Kabisa Yenye Ukweli 90% Kujua Kama Mtoto ni Wako Au Umebambikiziwa


Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena.

Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra.

Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao.

Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadala ( ukiachia ile ya kufanya DNA ambayo wengi wetu ndiyo tumeizoea ) ya Kiutamaduni ya kuweza kujua kama Mtoto aliyezaliwa na Mpenzi au Mke wangu ni wangu au nimebambikiwa.

Ndugu zanguni wana JF majibu niliyoyapata kutoka kwa hao Wazee wote yalinifanya nizidi kuamini kuwa kumbe tukiwatumia vizuri hawa Wazee bila kuwadhihaki, kuwadharau na kuwapuuza basi wanaweza kuwa sehemu yetu kubwa sana ya kupata maarifa na hata kutatua changamoto zetu zingine za kimaisha ambazo nyingi zimekuja kutokana na mfumo wetu huu wa Kimaisha ulioratibiwa na utandawazi ambao kimsingi umetuharibu na unaendelea kutuharibu.

Leo naweka hapa hadharani jinsi ya Wewe Mwanaume mwenzangu ambaye una Mtoto au hata upo mbioni kumpata Mtoto kuweza kujua kama huyo Mtoto aliyezaliwa ni wako kweli Kibailojia au umebambikiwa tu. Na nitangulize samahani kama kuna ambao nitawakwaza juu ya huu ukweli wa DNA ya Kiutamaduni ila nia yangu ni kuwaokoa tu Wanaume wenzangu juu ya hii kadhia ambayo imesababisha mitafaruku mingi mno katika Mahusiano na Ndoa.

HUU NDIYO UKWELI WA DNA YA KIUTAMADUNI

Ewe Mwanaume mwenzangu uliye na Mtoto hapo ulipo awe bado mdogo au tayari ameshakuwa Mtu mzima chukua mkono wowote uwe wa Kulia au wa Kushoto wa Mtoto unayeamini kabisa kuwa ni wako kisha kwa umakini kabisa huku ukiwa umetulia angalia pale katikati ya mkono ( katika palm ) linganisha ile mistari iliyopo na ya Mwanao kisha ukimaliza linganisha tena mistari iliyopo katika vidole vyake na vya Kwako.

Kwa mujibu wa hawa Mababu na Mabibi ( Wazee ) wanasema kuwa endapo Wewe Baba ukilinganisha hizo alama nilizokuelekeza hapo juu na kuona kuwa hazifanani na zako basi automatically jua ya kwamba huyo Mtoto siyo wako 100% na kwamba Mpenzi wako / Mkeo amekubambikia tu hivyo cha msingi tu ukishajua huu ukweli piga moyo konde, msamehe na maisha yaendelee.

Wamesema kwamba hata iweje Mtoto wako wa damu yako kabisa akizaliwa ni lazima tu alama zilizopo katika Mikono yake zitafanana na Wewe na wala haziongopi. Na ndipo hawa akina Babu na Bibi wakaenda mbele na kusema kuwa hiyo mbinu ndiyo iliweza kuwafanya wao huko nyuma wasiwe wasaliti na wawe wakweli kwani katika Makabila mengi hiyo mbinu ilishasambazwa na iliendelea kutumika. Na ili kulithibitisha hili ndiyo maana Bibi yoyote au Babu akipelekewa Mjukuu akimbeba tu kisirisiri atawahi kuuangalia mkono wa Mjukuu wake na hasa vidole vyake kisha atajua kuwa Mtoto wao kazalisha au kazalishiwa na wenzake.

MWISHO

Andiko langu hili kamwe halina kusudio la kuharibu Mahusiano yoyote yale bali naomba tulitumie tu kama sehemu ya kujipatia maarifa ambayo nina amini wengi wetu ( Vijana na Mabinti ) wa leo tulikuwa hatuna na kama itatokea umekuta umezalishiwa ( umebambikiwa ) basi ninachokuomba tu samehe, piga moyo konde na songa mbele na ule msemo wa Wahenga kuwa siku zote Kitanda hakizai haramu.

Kwa Dada zangu Wapendwa najua huu uzi utawaudhi na kuwauma ila tuvumiliane tu na pengine huu uzi unaweza ukawa msaada mkubwa sana Kwenu hasa katika kuwafanya mbadilike na muache kuwabambikia Wanaume zenu Watoto ambao siyo wao kwani hata Takwimu za mara ya mwisho za Mkemia Mkuu wa Serikali zinasema kuwa 49% ya Wanaume wa Kitanzania wanalea Watoto wasio wao ( wamebambikiwa ) hivyo mtusamehe na mtuonee huruma sisi Wanaume.

Nawasilisha.

BY GENTAMYCINE

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

9 comments:

 1. Viganja vya mkono kweli hutumika kama DNA katika suala la kuangalia ni mtoto wako aua la.

  ReplyDelete
 2. C kwel Ni uongo cos Watoto wote wangefanana..labda ungesema muoto WA nyele hapombele ya paji la uso

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ongezea nawe elimu yk badala ya kukimbilia uongo af yk uifanye siri

   Delete
 3. Sina hakika na utafiti wako kwani kuna utafiti wa ki-biolojia unahitisha kuwa kila binadamu duniani anazo finger print zake mwenyewe na hazifanani na mtu yeyote duniani kama walivyo pundamilia mnyama kuwa kila Puna milia mistali aliyonayo haifanani na punda milia mwingine ni ya kwake tu dunia nzima. Sasa hii uliyoileta ina weza kuleta shida kwa watu wasiyojua mambo haya ya kisayansi, lakini ulkienda mbele zaidi kuna LAW OF HERNIHERITENCE YA SIR DARWIN, ambayo inasemakuwa mtoto anaweza kufanana, na baba, mama,babu au hasifanane na wote akafanana na uzao wako ambao uenda ukuwahi kuwaona na hata babako au mamako hakuwahi kuwaona kwani ukoo unaanzia mbali sana, hivyo kwa njia hiyo ni ya mkato mno, kwani pia mtoto kwa vile mnagawana vinasaba na mama chrolosomes hili kupata mtoto huyo, ambapo kila mmoja utoa idadi 46, pia inawezekana alama za mkononi zikawa ni za mama, hapo itakuwaje,ingawa hapo kuna masuala ya Recessive na Dominant. Ni somo kubwa hadi kufikiria vinginevyo kuwa mtoto ni wako au siyo wa kwako, kwamfano kuna watoto wa kiume wanafanana sana na sura za mama zao na pia wa kike kufanana na baba zao, hapo inakuwaje? tusitafute njia za mkato hapa twaweza kuzalisha matatizo ambayo siyo ya lazima ikiwa ni pamoja na mauaji kwa wana ndoa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Darwin!!"the father of ignorance"

   Delete
  2. Darwin!!"the father of ignorance"

   Delete
  3. Hujaambiwa finger print na ww umeambiwa alama zilizopo katikat ya kiganja

   Delete
 4. Ni uongo.tumejaribu kuangalia mtoto na babu yake(baba)yetu kwani kuna mtoto tumeletewa kwenye familia yetu,na aliyemleta kazaa na kaka yangu ambae ni marehemu,mtoto anafanana na kaka yangu na hatukuwa na swali tangu siku kaletwa kwetu,baba wa mtoto ni chotara mama ni mweusi sana lakini mtoto kachukua kwa baba yake kila kitu,kucheka,kutembea,kuongea.Msije vunja ndoa zenu kwa huu upuuzi,ikibidi nendeni kitaalamu.

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger