Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kumpata Zuchu Kwaajili ya Show ni Tsh Million ishirini kwa Show Moja! Je Show Zake Zina Thamani Hiyo?

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Wasalaam!

Wana jamvi habari njema ni kwamba sanaa yetu imezidi kuchanja mbunga na kwa sasa muziki unalipa sana tena sana pamoja na kuwepo kwa madalali qengi!

Zuchu ni msanii mpya ndani ya WCB lakini ukuwaji wake umekuwa wa kasi sana ukilinganisha na wasanii wenzie wakina Lava Lava na Queen Doreen ambao kwangu mimi naona wamekuwa kama wafanyakazi hewa!

Hivi karibuni baada ya kufanya show yake kubwa pale Mlimanicity meneja wake Salam ametangaza bei ambayo atakuwa anatozwa mtu au kampuni au watu wanao mtaka Zuchu a.k. Chuchu kwenye show kiasi cha Tsh Million 20 za kitanzania!

Hivyo ni kwa sasa ukimtaka Zuchu itakubidi utoe Million 20!

Lakini sisi tunashauri Zuchu aendelee kuboresha ubora wa show zake ili azidi kuwakonga mashabiki wasione wanaibiwa hela zao!

Post a Comment

0 Comments