8/07/2020

Mary Mwanjelwa Ahojiwa Kwa Tuhuma za Kutoa Rushwa Kura za Maoni

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mary Mwanjelwa, amehojiwa na Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kutoa rushwa wakati wa kura za maoni.

Naibu Waziri huyo katika Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mary Mwanjelwa, amedaiwa kutoa rushwa kwa wajumbe wa Mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mbeya ili achaguliwe kuwa mgombea ubunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni baada ya simu yake kuvuja akiwa anaongea na mjumbe Kama amepokea pesa.

Matokeo Ubunge viti maalum Mbeya .
Mary Mwanjelwa - 374
Maryprisca Mahundi - 336
Suma fyamndomo -213
Mary Mbwilo - 199

#UchaguziMkuu2020
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger