8/16/2020

Mdogo wake Trump afariki duniaNdugu yake rais wa Marekani Donald Trump, Robert Trump, amepoteza maisha  hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu mjini New York.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye ametoa taarifa ya maandishi juu ya kifo cha kaka yake Robert Trump (72), amesema


"Kwa huzuni kubwa, kaka yangu mpendwa Robert amefariki kwa amani usiku wa kuamkia leo. Alikuwa sio kaka yangu tu, bali pia rafiki yangu mkubwa. Tutakukumbuka sana, lakini siku moja tutakutana tena."


Imeripotiwa kwamba Robert Trump, anayejulikana kwa msaada wake kwa Trump, alikuwa akitibiwa ugonjwa ambao haujafafanuliwa wazi.


Trump alimtembelea kaka yake jana, ambaye alipelekwa hivi karibuni katika Hospitali ya New York-Presbyterian huko Manhattan.


Hakuna taarifa yoyote ambayo imetolewa kutoka kwa mamlaka kuhusu sababu halisi ya kifo cha Robert Trump.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger