8/04/2020

Mondi, Zuchu Wana Lao JamboNI kizaaza cha aina yake kimeibuka kufuatia matukio mbalimbali waliyoyafanya msanii anayekuja kwa kasi kunako anga la Bongo Fleva, Zuhura Othman ‘Zuchu’ na bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linakusogezea mchapo kama wote!

MATUKIO MABICHI


Wikiendi iliyopita dada wa Diamond au Mondi, Esma Khan almaarufu Esma Platnumz alikuwa akifunga ndoa na mchumba wake, Yahya Msizwa nyumbani kwao Madale-Tegeta jijini Dar, wikiendi iliyopita ambako huko kuliibuka sintofahamu baada ya Mondi kuonekana yuko beneti na Zuchu muda mwingi na kuwafanya watu wajiulize na kubaki bila majibu.

Sintofahamu hiyo ilikwenda mbali zaidi kwa baadhi ya waalikwa kiasi cha kufi kia hatua ya kutaka kugombana kutokana na kubishana.

WADAI NI KUMKOSEA MONDI


Kuna ambao waligeuka mbogo kwa kusema kuwa, kudai Mondi anatoka kimapenzi na Zuchu ni kama kumtusi staa huyo kwani anaheshimiana vilivyo na mama mzazi wa binti huyo, Malkia Khadija Omari Kopa ‘Bi Khadija’.

“Hebu acha ujinga wako bwana au unataka nimwambie Mondi akutoe sasa hivi, unaongea upuuzi gani huo?”


Alisikika mmoja wa waalikwa aliyekuwa akibishana juu ya suala hilo na kuzua kizaazaa na kurushiana maneno makali. Mwenzake aliposikia kitisho hicho naye alikuja juu, lakini hata hivyo, alivyotishiwa kuwa atatolewa nje ya shughuli, akawa mdogo kama piritoni.

MATUKIO YALIYOCHAGIZA UTATA…


Tukio la Mondi kuonekana anaingia na Zuchu kwenye shughuli hiyo limekuwa ni tukio ambalo linazungumzwa mno kuwa huwenda kuna kitu kinaendelea baina yao.

Waalikwa hao walisema si mara ya kwanza kwa wawili hao kuingia pamoja kwenye shughuli mbalimbali, hata kwenye hafla ya Zuchu pale Mlimani City, Julai 18, mwaka huu ilikuwa hivyohivyo. Siku hiyo, Mondi aliingia akiwa amemshika mkono Zuchu na kupiga picha za pamoja kwenye zulia jekundu kama ilivyofanyika Madale.

TUKIO LA KUCHEZA PAMOJA


Kwenye usiku wa Maulid ya harusi hiyo ya Esma, Zuchu na Mondi walionekana wakicheza muziki pamoja kama ‘mista’ na ‘misezi’, kitendo ambacho kilifanya watu kuunganisha matukio kuwa, kuna kitu kinaendelea hapo kati maana mwanadada alikata kiuno kwelikweli.

Tukio hilo limekuwa likizungumziwa kiasi cha kuwachanganya mashabiki wao na kuwafanya waendelee kuhisi kuwa wawili hao wana lao jambo kwani si jambo la kawaida kwa bosi na mafanyakazi wake kuwa na mazoea kiasi hicho kama ilivyo kwa Zuchu na Mondi.

MAVAZI YAO…


Kufanana kwa mavazi yao siku ya shughuli ya Esma, nako kulisababisha watu kuibua ubishani kati yao.

MATUKIO MENGINE


Matukio mengine mbali la shughuli ya Esma ni pamoja na;

ZUCHU KULALA KWA MONDI


Tukio hili lilizua gumzo mno baada ya kusikika tetesi kuwa Zuchu analala kwa Mondi yaani pikapakua. Hata mama mzazi wa Zuchu, Bi Khadija alikiri kuwa ni kweli mwanaye analala kwa Mondi, lakini si kwa ubaya ni kwa ajili ya kazi tu na si vinginevyo.

TUKIO LA SHOPPING


Tukio la Mondi kumfanyia Zuchu shopping ya mamilioni imekuwa ni gumzo lingine ambalo linawaacha watu midomo wazi. Aprili, mwaka huu, Mondi alifanya kufuru kwa kumfanyia Zuchu shopping ya kutosha.

Kama hiyo haitoshi, hivi  karibuni kabla ya shoo ya Mlimani City, Mondi na Zuchu walionekana Mitaa ya Sinza-Madukani jijini Dar kwenye Maduka ya Vunja Bei wakiuza tiketi na baada ya hapo walifanya shopping ya kutosha.

KUMZAWADIA GARI…


Tukio lingine lililoibua maswali ni lile la bosi huyo wa Wasafi kumzawadia Zuchu ndinga kali aina ya Toyota Vanguard kupitia Show ya Big Sunday Live ya Wasafi TV, jambo ambalo hajawahi kulifanya kwa msanii wake mwingine.

Zawadi hiyo ilitolewa ndani ya saa 24 tangu Zuchu afanye shoo kubwa yenye mafanikio makubwa ndani Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ya kuwashukuru mashabiki wake kwa mapokezi makubwa waliyompatia kwa kipindi kifupi alichokuwepo kwenye muziki.


 


Matukio mengine ni kule Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa CCM, ambako wasanii wengi walialikwa. Zuchu na Mondi walionekana kuwa pamoja muda wote walipokuwa mjini Dodoma.

ZUCHU NI NANI?


Zuchu ni msanii wa pili wa kike kusainiwa kwenye Lebo ya Wasafi baada ya dada yake Mondi, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.

Tangu Zuchu asajiliwe hivi karibuni, amekuwa akipewa kipaumbele kimuziki na Mondi, jambo ambalo limezua maswali na wengine kumsihi Zuchu kuwa makini, asije akaingia kwenye himaya ya mapenzi ya msanii huyo kwani mwisho wake hautakuwa mzuri.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger