8/28/2020

"Nashangaa Hawaniweki kwenye orodha ya Wasanii Bongo Wenye Elimu" Chemical


Rapa wa kike Bongo Chemical Mwana wa lubao, amesema anashangaa kwanini hawamuweki kwenye orodha ya wasanii wenye elimu hapa nchini Tanzania wakati vyeti vyake vipo vizuri na amesoma hadi kufikia ngazi ya juu kabisa.


Chemical amesema kuna siku aliona story inayohusu wasanii wenye elimu kwenye mtandao wa Youtube lakini alishangaa hakuwekwa kwenye orodha hiyo ila akagundua kuwa mtu akiwa na elimu mpaka ajitangaze.

"Nashangaa sana niliwahi kuangalia YouTube nikakuta baadhi ya wasanii wamewekwa kuwa ndiyo wenye elimu ya juu halafu mimi hawakuniweka nilishangaa sana, nikagundua elimu ya mtu mpaka mtu mwenywe aseme" amesema Chemical 

Pia ameongeza kusema ''Elimu yangu ni ya juu hata vyeti vyangu sio vibaya, nisingekuwa UDSM kama vyeti vingekuwa vibaya na sijapata division four, nipo vizuri".

Kibongobongo baadhi ya wasanii ambao wanatajwa kwamba wamefika mbali kielimu ni Nikki wa Pili, Mwana Fa, Wakazi, Cpwaa, Mike T na wengineo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger