Sakata la Morrison Maamuzi Leo Yakwama..Watu Warundikana Kusubiria Maamuzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KIKAO cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti, Elias Mwanjala, kimemalizika jioni hii ya leo.

Agosti 10 kulikuwa na kesi ya kuskilizwa kuhusiana na suala la kiungo mchezaji wa Yanga ambaye yupo kwenye mvutano na uongozi wa timu yake kwenye suala la mkataba.


Kuanzia asubuhi ya leo mpaka jioni kikao kilikuwa kikiendelea  lakini hakuna maamuzi yoyote rasmi yaliyotangazwa kwa Waandishi wa Habari waliokuwepo viunga vya TFF, Karume, Jijini Dar Es Salaam.


Wadau wengi wa masuala ya michezo walijitokeza makao makuu ya TFF hali iliyopelekea Polisi kuingilia kati kuweka ulinzi na usalama kwa raia.


Mvutano mkubwa upo kwenye mkataba ambapo mchezaji anasema kuwa alisaini kandarasi ya miezi sita huku Yanga wakieleza kuwa alisaini kandarasi ya miaka miwili.


Agosti 8, saa nane, Simba ilimtambulisha mchezaji huyo kuwa mali ya Simba jambo ambalo liliamsha hisia kwa Yanga ambao walitoa taarifa kwamba wanalifuatilia suala hilo kwa ukaribu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad