8/14/2020

Serikali ya Afghanistan yawaacha huru wafungwa 80 wa TalibanSerikali ya Afghanistan imeanza kuwaacha huru wafungwa wa mwisho wa kundi la Taliban kutoka kundi la wafungwa 400 ambao wanamgambo hao wanataka waachiwe kabla ya kukubali kuanza majadiliano ya amani.
Serikali imekubali siku ya Jumapili kuwaachia huru wafungwa sugu 400 baada ya ushauri kutoka katika baraza la wazee pamoja na viongozi wengine wa jamii, linalofahamika kama Loya Jirga.

Msemaji wa baraza la usalama la taifa, Javid Faisal amesema serikali jana iliwaacha huru wafungwa 80 wa Taliban kutoka idadi ya wafungwa 400 ambao Loya Jirga imeidhinisha kuwachia, ili kuharakisha mazungumzo ya moja kwa moja na kusitisha mapigano nchi nzima.

Hata hivyo, hakusema lini kundi lingine la wafungwa 320 litaachwa huru.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger