Shilole: Nimemalizana na Uchebe, Nikipata Mume Naolewa


MSANII wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au ‘Shishibaby’ ameweka bayana kuhusu alivyomsaidia aliyekuwa mume wake, Uchebe , kumfungulia biashara na kumtengenezea heshima kwa familia yake na jamii licha ya ndugu wa Shilole kumchukia mwanaume huyo.

Shilole ameanika hayo jana Jumatano, Agosti 12, 2020, usiku wakati akifanya mahojiano na Clouds TV kuzungumzia maisha yake na namna alivyopambana mpaka kufika hapo alipo leo.

“Nilijishusha sana kwa Uchebe, nilitumia nguvu zangu kum-brand, nilimheshimu sana bila kujali kipato chake. Nimemkuta ana followers watatu Instagram, ndugu zangu hawakutaka kabisa niolewe nae. Pesa ya mtaji wa spare za gereji nimempa mimi, alikuwa anapiga picha kwenye maduka ya watu hata ufundi bado hajajua vizuri.

“Uchebe hajawahi kunifumania, lakini kwa kipigo hapana. Kaka yangu Makonda ametusuluhisha sana na anakiri kabisa anasema sirudii tena lakini bado ananidunda tu. Mshika dini gani anampiga mke wake vile, tena wakati mwingine mbele ya watoto wangu kabisa?

“Ndugu zangu hawakutaka niolewe na Uchebe lakini mimi nililazimisha, kumbe walijua wameoma kwamba haya yatatokea, nakumbuka dada yangu mkubwa alikataa kabisa mimi kuolewa na Uchebe mpaka akalia ana galagala kwangu, nikamtia polisi wakaja kumtoa.
“Mke wa Babu Tale (marehemu) ndiye alikuwa akifua damu zangu nikipigwa na Uchebe, akikudunda wala hakutibu hata kuuliza unaendeleaje hakuna. Alivyonipiga mara ya mwisho aliniumiza sana, mpaka sasa kifua changu kinanisumbua, nilipima nikaambiwa kuna shida, kesi nilipeleka polisi, muda si mrefu itakuwa mahakamani, nitapambana mpaka nipate haki yangu.

“Kuanzia leo nimefunga kabisa ukurasa, sitamzungumzia tena Uchebe, nimeshamwambia adhabu yake ataikuta kwa Mungu. Mimi ni mwanamke, nisiseme uongo, nikipata mwanaume ambaye tutapeana kila mmoja anachokihitaji nitaolewa, lakini sio sasa, ni mpaka baadaye,” Shilole.
That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments