8/31/2020

Tanzania Yatajwa Nchi ya Kwanza kwa Amani Afrika MasharikiJAMHURI ya Muungano wa Tanzania imetajwa kuwa ndiyo nchi ya kwanza (inayoongoza) kwa kuwa na amani katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa jarida la Kimataifa la Global Peace Index limetoa takwimu za mwaka 2020 zikionyesha kuwa Tanzania imepanda juu huku ikiwa ya sita kwa Afrika na ikishika nafasi ya 52 duniani kote.

Kwa mujibu wa jarida hilo,  eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara limepungua kwa kiasi kidogo mazingira ya amani na usalama kwa asilimia  0.5.Nchi 20 katika eneo hilo zimeimarika kiwango chake cha amani na lakini nchi 24 zimepungua kiwango chake cha mazingira ya amani.

Migogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi na madai ya kuwepo mabadiliko ya kisiasa, yamesababisha machafuko na vurugu za kisiasa katika nchi kadhaa eneo hilo ikiwa ni pamoja na maandamano ya vurugu mnamo mwaka uliopita.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger