8/09/2020

Timu Samatta Yachapwa Mabao 3-1 Na Timu Kiba, Morrison Akosa PenaltiTIMUKiba leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya TimuSamatta kwenye mchezo wa hisani wa SamaKiba Foundation uliochezwa Uwanja wa Mkapa.Lengo la mchezo wa leo ni kurejesha kile wanachokipata kwa jamii ambapo mchezo wa leo ulikuwa ni wa tatu kwa TimuKiba na TimuSamatta kukutana huku mechi zote mbili zilizopita ushindi ulikuwa ni kwa TimuSamatta hivyo leo TimuKiba imepata ushindi wa kwanza.


Mabao ya upande wa TimuKiba yalifungwa na Ibrahim Ajibu  dakika ya 25,Mudhathir Yahya dakika ya 53 na la tatu lilipachikwa na Hassan Dilunga dakika ya 90.

Bao pekee la TimuSamatta lilifungwa na Yahaya ambaye alijifunga dakika 59.


TimuSamatta walipata penalti mbili zote zilipigwa na Bernard Morrison ambaye alikosa penalti ya kwanza baada ya kumpa pasi Idd Naldo aliyepaisha na ile ya pili Morrison aliipaisha mwenyewe.

Kiba amesema kuwa ni furaha kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi huku akiwaomba waendelee kutoa sapoti.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger