8/12/2020

Tundu Lissu Adai Kupokea Vitisho Vya KuwawaMgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema amekuwa akipokea taarifa nyingi za vitisho vya kifo tangu juzi (Jumapili) na kuwataka Wanachama kuwasindikiza wagombea Ubunge na Udiwani NEC kuchukua fomu.

Akizungumza na wakazi wa mkoa wa Singida ambako yupo kwa nia ya kitafuta wadhamini kabla ya kurejesha fomu za kugo,nea urais kwenye uchaguzi mkuu mapema mwezi Oktoba Lissu amesema sasa sio muda wa kutishana na wajibu wa vyombo vya usalama kuwalinda watu wote.

“Katika mazingira ya kawaida ningeweza kusema hivi ni vitisho tu, lakini hatuishi tena katika mazingira ya kawaida. Tangu Septemba 07, 2017 na yale marisasi yote yale hatuwezi tukapuuzia tena kitisho chochote, Huu sio muda wa kutishana tena, huu ni muda wa Uchaguzi wananchi wa Tanzania wapate viongozi wanaostahili” amesema.

Lissu ameeleza kuwa jukumu na wajibu wa kisheria wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kuhakikisha wanaopanga mipango ya mauaji wanachukuliwa hatua zinazostahili.

CHANZO: JAMIIFORUMS
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger