Wakaazi wa mji wa Beirut waonyesha ghadhabu dhidi ya serikali, wataka majibu kuhusu mlipuko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakaazi wa mji wa Beirut sasa wameonyesha ghadhabu dhidi ya serikali kuhusu kile wanachosema ni uzembe uliosababisha mlipuko mkubwa siku ya jumanne. Wengi wamelaumu serikali kwa ufisadi, uzembe na usimamizi mbaya.'Beirut inalia , Beirut inapiga kilele, watu wamechoka, mtengeneza wa fimau Jude Chehab aliambia BBC, akitaka watu waliohusika kukabiliwa kisheria.Chadia Elmeouchi Noun, mkaazi wa Beirut alie hospitalini, alisema: Nimejua wakati wote kwamba tunaongozwa na watu wasioweza kuongoza, lakini nakwambia kitu kile walichofanya sasa ni uhalifu mkubwa.


Aidha, baadhi ya maafisa wa mji wa Beirut wamewekwa katika kifungo cha nyumbani huku wakisubiri uchunguzi kuhusu mlipuko mkubwa wa siku ya Jumanne, kulingana na serikali ya Lebanon.

Mlipuko huo uliwaua watu 135 na kuwajeruhi wengine 4000. Hali ya tahadhari ya wiki mbili imeanza kutekelezwa nchini humo.

Rais Michel Aoun alisema kwamba mlipuko huo ulisababishwa na tani 2750 za Amonium Nitrate iliokuwa imehifadhiwa katika ghala moja katika bandari ya mji huo.

Afisa mkuu wa masuala ya forodha Badri Daher alisema kwamba shirika lake lilitoa wito kwa kemikali hiyo kuondolewa, lakini hilo halikufanyika.

''Tumewaachia wataalamu kufichua sababu zake'', alisema. Amonium Nitrate hutumika kama mbolea katika kilimo na pia kama kilipuzi.

Katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri siku ya Jumatano, rais Aoun alisema: Hakuna maneno yanaweza kuelezea tishio ambalo limekumba Beirut usiku uliopita, na kuufanya mji huu kama uliokumbwa na janga.

Wataalamu katika chuo kikuu cha Sheffield nchini Uingereza wanakadiria kwamba mlipuko huo ulikuwa na kiwango cha 1/10 cha nguvu za bomu la nyuklia lililoangushwa katika mji wa Japan wa Hiroshima wakati wa vita vya pili vya dunia na limetajwa kuwa mlipuko mkubwa wa bomu lisilo la nyuklia katika historia .
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad