8/18/2020

Wazir Junior Aahidi Mabao 30 Yanga SCSTRAIKA mpya wa Klabu ya Yanga, Wazir Junior, amefunguka kuwa mipango yake katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ni kuifungia timu hiyo mabao 30 na kuweka rekodi yake katika timu hiyo.

Wazir amesema anafahamu kuwa wachezaji wengi waliopata nafasi ya kucheza timu kubwa wakiwa wametokea timu za kawaida, hukutana na changamoto za kufanya vizuri ila kwa upande wake amejipanga kufanya makubwa ndani ya timu hiyo.


Wazir amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mbao FC. Wazir alimaliza msimu wa 2019-20 akiwa kinara wa mabao ndani ya Mbao akiweka kambani mabao 13.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Wazir alisema yeye anatambua kilichofanya atue Yanga ni kufunga mabao, hivyo hatafanya makosa katika hilo na atafunga mabao 30 kama Mungu atamuongoza na kumpa nguvu ya kupambana.

“Najua wachezaji wengi hufeli pindi wanapojiunga na timu kama Yanga, kwangu mimi itakuwa tofauti kwa sababu najua nini kimefanya nisajiliwe na timu hii. Nitafunga mabao 30 kama Mungu atanisimamia,” alisema Wazir.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger