8/28/2020

Yanga yafunguka hatma ya Juma Abdul, Yondani INJINIA Hersi Said, Mkurugenzi wa Masuala ya Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa timu hiyo imefunga hesabu za wachezaji wa ndani na mpango uliopo ni kuboresha kikosi kwa kuleta wachezaji wa kimataifa.

Ilikuwa ikielezwa kuwa Yanga ipo kwenye mazungumzo na nyota wao wa zamani, Juma Abdul na Kelvin Yondani ambao mikataba yao ilikwishwa na walishindwana kwenye masuala ya kuongeza mikataba upya.


Hersi ameweka wazi suala hilo kwa kusema kuwa:"Hakuna hesabu za kuwaleta wachezaji wa ndani kwa sasa kwa kuwa tayari tumeshafunga hesabu zao hivyo hatuna mpango wa kuwasajili wachezaji ambao tulishaachana nao.


"Ni wachezaji wazuri na tunawaheshimu lakini hakuna nafasi ndani ya Yanga, kwa sasa tunafikiria kuleta wachezaji wakigeni ili kufunga mjadala wa kuleta wachezaji na kufanya maandalizi mengine ndani ya timu," amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger