Ticker

6/recent/ticker-posts
.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREGari la msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe, Andrew Kadege limezama katika mto Momba wakati wakitokea katika kijiji cha Nsyanza kuelekea makao mkuu ya Kata ya Chilulumo mkoani humo.


 


Gari hiyo aina ya Jeep namba T 923 DJQ lilizama katika mto huo muda wa saa tano usiku huku ndani yake kukiwa na watu wanne wakiwamo viongozi wa UVCCM mkoani humo.


 


Akisimulia mkasa huo Mratibu wa kampeni za UVCCM mkoa humo ambaye pia alinusurika katika tukio hilo, Ombeni Nanyaro alisema baada ya kumaliza mikutano ya kampeni na kwenda kuzungumza na wananchi wa Kijiji  hicho cha Nsyanza, muda wa saa tano walianza safari ya kurejea makao makuu ya kata Chilulumo.
“Ndani ya gari nilikuwepo mimi, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Songwe Andrew Kadege, Mwandishi wa habari Raheem Secha pamoja na dereva.


 


“Tulipofika karibu na mto huo, mbele yetu kulikuwa na gari ndogo ambayo ilivuka salama maana hapakuwa na maji mengi. Katika mto huo gari huvuka kwa kukanya ndani ya mto kwani hakuna daraja zaidi ya daraja dogo la watembea kwa miguu ambalo lipo kando.
“Kwa hiyo magari huvuka tu pale ambapo hakuna maji mengi, lakini tulipoanza kuvuka sisi na gari yetu ghafla maji yaliongezeka, gari likatitia na mwishowe likazama.


 


“Wakati maji yanakaribia kufunika madirisha ya gari ndipo tulihangaika kupiga kelele huku tukipiga simu wenzetu waliopo kijijini hapo na bahati nzuri wananchi walijitokeza na kutusaidia kulinasua gari na sisi tukiwa ndani yake,” alisema.
Alisema baada ya wananchi kunasua gari hilo mtoni, viongozi hao walitoka salama ndani ya gari hilo ambalo sasa limeharibika baadhi ya vifaa.


Aidha, Mwenyekiti wa UVCCM – Songwe, Andrew Kadege alimshukuru Mungu kwa kuwa wamenusurika ajali hiyo ambayo wametoka salama.


 


“Kwa nguvu za mwenyezi Mungu tunaendelea na mapambano mpaka kieleweke, lengo letu ni kuhakikisha CCM inachukua majimbo yote Songwe mgombea wetu wa urais Dk. Magufuli anapata kura za kutosha,” alisema Kadege


Hata hivyo, Kadege alisema baadhi ya wananchi waliofika kuwaokoa, wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
“Kwa sababu wakati wanalivuta gari, lilinasa kwenye mchanga ambao upo chini ya maji hayo ya mto na baada ya kutoka tu, wanadai alitoka paka chini ya siti ya dereva na kukimbia.


“Wanadai kuwa awali paka huyo walimuona akiwa amebebwa kichwani na kijana mmoja ambaye muda wa mchana walimfukuza kijijini hapo kutokana na kuhusishwa na imani za kishirikina,” alisema.

Post a Comment

0 Comments