JPM: Tunapeleka umeme hata kwenye nyumba za nyasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa serikali yake haibagui aina ya nyumba katika kuwaunganishia wananchi umeme, hata nyumba iwe ya nyasi. Amesema hayo  akiwa katika muendelezo wa kampeni zake alipokuwa Igalula (Tabora) njiani kuelekea Itigi (Singida).


''Tunapeleka umeme hata kwenye nyumba za majani sawa, lakini tungependa zaidi tupeleke umeme kwenye nyumba za bati na hiyo ndiyo Tanzania ninayotaka kuijenga'' amesema Magufuli.


Aidha Magufuli amewataka wananchi kujitahidi na kutamani zaidi kujenga nyumba za bati na zenye ubora kwa kujiwekea malengo na akiba kwa kipindi husika pasipo kuogopa bei za dhana za ujenzi ama kusikiliza maneno ya watu.


''Ukipata hela yako jenga nyumba nzuri, nataka niwaeleze hilo hata ukipata Sh 10,000 nenda kanunue bati, chukua matofali yako anza kuyafyatua maudongo yapo tena udongo mzuri tu sio lazima ufyatue matofali ya 'block' '', amesema Dkt Magufuli.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad