9/04/2020

"Kodi milioni 4 kwa mwezi, nina pesa" - Gigy Money


Staa wa kike wa BongoFleva Gigy Money amefunguka kuwa ana pesa za kumlisha miaka ijayo hata kama asipofanya kazi, pia amesema analipa kodi ya milioni nne  kwenye nyumba yake.

Akizungumza kwenye show ya eNewz ya East Africa Tv, Gigy Money amesema pesa hizo anajilipia mwenyewe tena bila ya kudanga au kutumia pesa ya mwanaume.

"Mimi ninafanya kazi zangu na najituma hakuna hata mwanaume nyuma yangu msije mkajidanganya kama nadanga, ninalipa kodi ya Milioni nne kwa mwezi, mimi sio mwanamuziki pekee bali ni mburudishaji, nina ushawishi na balozi nina pesa ambayo nimelipwa na zinaweza kunilisha miaka" amesema Gigy Money
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger