Kuhusu Morisson mtanyamaza wenyewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KOCHA  msaidizi wa Simba Seleman Matola,  amemwagia sifa winga mpya wa timu hiyo Bernard Morrison.


Matola kiungo na nahodha wa zamani wa mabingwa hao mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara alisema Morisson ni mchezaji wa daraja la juu na ataisadia timu hiyo kwenye ligi na michuano ya kimataifa.


Morrison aliyejiunga na Simba wakati wa dirisha kubwa la usajili bado hajaonyesha makali yake kwenye mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu dhidi ya Ihefu na Mtibwa Sugar lakini Matola alisema ni suala la muda tu na mashabiki wa Simba watafurahia.



 

Alisema amekuwa akimfuatilia kwa karibu winga huyo wa zamani wa Vita Club na Orlando Pirates na kubaini ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na akija kuzoeana na wenzake mabeki wa timu pinzani watakuwa na shughuli pevu kumzuia.


“Huyu jamaa nimekuwa nikimfatilia tangu yupo Yanga, ukweli jamaa ana uwezo mkubwa halafu ana utundu fulani ambao kwenye miguu yake,”alisema Matola.


Matola alisema Morrison anapokuwa fiti huwa hana presha kwani kwa uwezo na kasi aliyokuwa nayo pindi anapokuwa na mpira ni ngumu sana kumzuia.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad