9/19/2020

Magufuli atoa wito kufuatia ufunguzi wa Mahakama

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ametoa wito kwa majaji na watumishi wa mahakama kuu ya kanda ya kigoma kutumia miundombinu ya mahakama hiyo vyema.


Ametoa wito huo leo Septemba 19, katika ufunguzi wa jengo la mahakama hiyo ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.


"Napenda kutoa wito kwa majaji na watumishi kutunza miundombinu iliyojengwa, waswahili wanasema kitunze kidumu natoa wito kwa majajai kuhakikisha mahakama hii inatimiza malengo yake ya kujengwa" alisema Rais Magufuli


Aidha kwa upande wake, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, ameshukuru kwa nafasi aliyopewa ya kufungua jengo hilo huku akisema ni jambo la heshima sana kwake


"Ni heshima kabisa kwa mimi kuwa hapa na kunikubalia kufungua jengo hili zuri sana na hekima kubwa kwangu nawashukuru sana" amesema Rais Evariste Ndayishimiye

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

  1. Karibuni kujimwambafai katika Ulimwengu wa fasihi
    https://www.mrbunduki.com/

    ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger