9/19/2020

Ndege ya mizigo imeanguka Somalia

Ndege ya mizigo imeanguka katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Mogadishu, Somalia. Hata hivyo hakujaweza kupatikina uthibitisho wa haraka wa athari zake ingawa picha zilizosambazwa zikielezwa kupigwa katika eneo la tukio zilionesha eneo la mbele la ndege hiyo likiwa limegonga ukingo ambao upo hatua chache kutoka baharini. 

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden Adde. 


Alama zilizomo katika ndege hiyo zinaonesha inaendeshwa na kampuni ya usafiri wa anga ya Kenya ya Silverstone.


 Hata hivyo msemaji wa mpango wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wa Somalia ambae alionekana katika picha za ajali hiyo, hakuweza kupatikana mara moja ili kuweza kutoa maelezo zaidi kufuatia ajali hiyo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger