Mazungumzo ya Baba yake Messi na Barcelona yachukua siku ya pili, wengine sokoni hawa hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Baba yake Lionel Messi amejadiliana na Barcelona kwa siku ya pili mfululizo juu ya uwezekano wa kijana wake kuhama klabu hiyo.

Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, anaonekana kuwa tayari kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu. (Mirror)

Manchester United inajaribu kumaliza suala la mshahara na kima cha uhamisho kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho kabla ya kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Star)

Manchester United inajaribu kumaliza suala la mshahara na kima cha uhamisho kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho

Sevilla ina matumaini ya kuendelea kuwa na beki wa Real Madrid Sergio Reguilon kwa mkopo kwa msimu mwingine licha ya Mhispania huyo, 23, kuhusishwa na uhamisho wa kudumu kwenda Manchester United. (Marca – in Spanish)

Arsenal inakaribia kukamilisha makubaliano ya mkopo ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Dani Ceballos kwa msimu wa pili. (Mail)

Arsenal inafikiria kumtafuta kiungo wa kati wa West Ham, MBrazil Felipe,27, Anderson. (Football Insider)

Liverpool haitakubali kiungo wa kati wa Welsh Harry Wilson, 23, kuondoka tena kwa mkopo licha ya Newcastle, Leeds na Southampton kuonesha nia ya kutaka

Chelsea imearifiwa kwamba lazima ilipe paundi milioni 30 kumsajili mlinda lango wa Senegal Edouard Mendy, 28, kutoka Rennes. (Telegraph)Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, anaonekana kuwa tayari kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu

Inter Milan itahitajika kutafuta pesa kwa kumuuza kiungo wa kati wa Croatia Ivan Perisic ikiwa itataka kutoa ofa kwa mchezaji wa Chelsea, 29, na kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Crystal Palace, West Ham, West Brom, Norwich na Watford zinamnyatia mlinzi wa Ufaransa, 26, Jean-Claude Billong, anayecheza katika ligi ya Serie B Salernitana. (Teamtalk)

Roma inafikiria kumchukua mshambuliaji wa Hertha Berlin na Poland Krzyszt wa Piatek kuchukua nafasi ya Edin Dzeko. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Hull City inatafuta kumsajili beki wa kati wa Southampton Alfie Jones, 22, kwa mkataba wa kudumu. (Yorkshire Post)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Mhispania Javi Martinez, 32, amedhamiria kufikia makubaliano kurejea Athletic Bilbao msimu huu. (Goal)
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad