9/30/2020

NEC: Kosa kubandika bango kwenye nyumba za watu

 


Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Mpiga Kura, kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Monica Mnanka, amesema kuwa mabango yote ya wagombea yanayopandikwa kwenye nyumba ya mtu lazima wahusika wawe wameridhia vinginevyo itakuwa ni kosa na mhusika ana haki ya kuyaondoa.

 

Akizungumza leo kwenye mahojiano katika kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio Mnanka amesema kuwa yapo maeneo ambayo mabango ya wagombea yanaweza kuwekwa kwa mujibu wa sheria.

 

“Kama bango umeweka kwenye nyumba ya mtu awe ameridhia kama hajaridhia hilo ni kosa, na pia kubandua bango la mgombea katika sehemu iliyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria faini yake si chini ya shilingi elfu thelathini, “ alisema Mnanka.

 

Aidha, Mnanka amesisitiza kuwa Mtanzania yeyote ambaye ni mpiga kura haruhisiwi kuharibu mabango ya mgombea yeyote kwani kila mgombea ana nafasi ya kunadi sera zake katika kipindi chote cha kampeni.

 

"Mpiga kura anatakiwa asiharibu mabango ya vyama au mgombea mwingine hatakama hukipendi kwa sababu kila chama kina fursa ya kutangaza sera zake na kunadi ilani ya vyama vyao," alisema Mnanka.

 

Pia Mnanka ameviasa vyama vya siasa kutumia Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi kutoa malalamiko yao ili yajadiliwe na kufanyiwa kazi badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari kwani tume inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger