Rais aliyepinduliwa wa Mali apelekwa nje ya nchi kwa matibabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais aliyepinduliwa wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, amesafirishwa kupelekwa Umoja wa Falme za Kiarabu kutibiwa. 


Mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa jina lakini anafahamu tukio hilo, amesema hayo na kuongeza kwamba Keita ameondoka akiwa pamoja na mke wake, madaktari wawili, mawakala wanne wa kiusalama na msaidizi. 


Tangu Keita mwenye umri wa miaka 75 alipolazwa hospitalini, baada ya kuwekwa kizuizini kwa siku 10 na wanajeshi waliompindua, maswali mengi yameulizwa kuhusu hali yake ya afya. 


Katika tukio jingine, mazungumzo kuhusu utakaokuwa utawala wa mpito nchini Mali yameanza jana Jumamosi mjini Bamako. Mamia ya wawakilishi wa vyama vya kisiasa pamoja na makundi ya kutetea haki za binadamu walihudhuria ufunguzi wa mazungumzo hayo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad