Rais: Sikuwa Tayari Kumuachia Lionel Messi Aondoke La Liga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



RAIS wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, Javier Tebas


RAIS wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, Javier Tebas, amesema kuwa kwao ilikuwa ni ngumu ku-muachia mchezaji staa wa ligi hiyo, Lionel Messi aondoke.

Messi alishatangaza kuondoka kwenye ligi hiyo na kwenda Manchester City, lakini ghafl a alibadilisha mawazo na kuamua kubaki kwenye timu hiyo baada ya majadiliano marefu na klabu yake.

Messi aligoma kufanya mazoezi kwa wiki nzima na Barcelona na juzi ndiyo alikwenda uwanjani kwa mara ya kwanza kuungana na timu hiyo.

Rais huyo amesema alipambana mwenyewe kuhakikisha kuwa mshambuliaji huyo bora duniani anabaki kwenye ligi hiyo.

Wakati Messi akisema kuwa anaondoka bure, La Liga walitoa taarifa iliyokuwa ikionyesha kuwa ili kumpata mchezaji huyo unatakiwa kutoa kitita cha pauni milioni 630, sawa na shilingi trilioni 2.

“Kama ligi lazima tulinde sheria na kufuata haki, kila mchezaji lazima aheshimu mkataba wake.


“Ukweli mimi sikuona mpambano kati ya Messi na klabu yake, kwanza natakiwa kumheshimu sana kwenye hilo na jinsi alivyokaa kwenye ligi hii kwa muda mrefu.

“Namheshimu sana Leo, nampenda sana na historia aliyotengeneza hapa kwa miaka 20 inajionyesha.

“Nafi kiri suala langu lilikuwa kuwa mkataba unaoheshimiwa, lakini vizuri pia ni kwamba walikaa wenyewe na kukubaliana na yote yakaisha, lakini kwangu ilikuwa mgumu kumuona anaondoka kwenye La Liga,” alisema rais huyo.

Ukweli ni kwamba La Liga ilikuwa inapambana kuona kuwa staa huyo anabaki baada ya kuondoka kwa Cristiano Ronaldo 2018.Messi juzi Jumatatu alikwenda mazoezini kwa mara ya kwanza na kukutana na kocha mpya wa timu hiyo, Ronald Koeman.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad