Rais wa DRC ataka mataifa masikini kusamehewa mzigo wa madeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameomba mataifa tajiri kutoa msamaha wa madeni kwa mataifa masikini yanayoendelea kupambana na janga la Corona.


Tshisekedi amesema hatua hii itasaidia mataifa hayo kama DRC, kuendeleza uchumi wake baada ya janga hili ambalo limeleta madhara makubwa ya kiuchumi katika mataifa masikini na yanayoendelea hasa barani Afrika,wakati nchi yake ikiwa na maambukizi zaidi ya Elfu 10 ya Corona.


Licha ya mataifa tajiri zaidi ya 20 na Shirika la Fedha Duniani, IMF, kusema kuwa yanatathmini cha kufanya kuyasaidia mataifa hayo, rais Thsisekedi katika ujumbe wake kwa viongozi wa dunia kupitia njia ya video, ametaka kufutwa kabisa kwa madeni hayo.


Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo linadaiwa kuwa miongoni mwa mataifa masikini duniani licha ya utajiri wake wa rasimali na imekuwa ikitegemea misaada ya mikopo kutoka nchi jirani kuendesha uchumi wake.


Suala la ukosefu wa usalama, hasa Mashariki mwa nchi hiyo na uongozi mbaya katika miaka iliyopita, zinaelezwa kuwa chanzo kikubwa cha umasikini huo.

OPEN IN BROWSER

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad