Rekodi za Cristiano Ronaldo zitakavyotawala Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Cristiano Ronaldo amefikisha magoli 101 tangu aanze kuichezea timu ya Taifa ya Ureno baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo wa mashindano ya mataifa yaliopo chini shirikisho la soka barani Ulaya , katika ushindi wa bao 2-0 walioupata kwa Sweden



Rekodi hiyo inamfanya kuwa mcheza wa pili kinara wa  mabao kwa timu za Taifa nyuma ya  mchezaji wa zamani wa  Iran  Alli Daei mwenye mabao  109 kutokana na michezo  149 aliyoitumikia  Taifa lake huku Ronaldo akifikisha magoli hayo 101 katika michezo 165

Ronaldo alianza kuitumikia timu ya Taifa  ya Ureno mwaka  2004  katika michuano ya bara la Ulaya maarufu kama ( EURO) ambapo Ureno  walikuwa wenyeji akiwakuta wachezaji wengi wakubwa na maarufu katika timu hiyo akiwemo Luis Figo , Manuel Rui Costa  Nuno Maniche na wengineo wengi .  Alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza katika mchezo dhid ya Ugiriki 12/6/2004

JE RONALDO ANAWEZA KUIPIKU REKODI YA  MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE  KWA TIMU ZA TAIFA?

 Uwezekano ni mkubwa sana licha ya umri wake wa sasa wa miaka 35, anaonekana kuwa bado na nguvu na kwa yale bora aliyoifanyia Taifa lake bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kuitwa katika kikosi hicho , anahitajika magoli 8 zaidi ili kufikia  rekodi za Alli Daei huku akihitajika goli  9 kuipiku rekodi hiyo ya  muda wote ya magoli 109

Takwimu zinaonesha kadri  umri unavyokwenda mbele zaidi ndio kiwango chake kinavyozidi kuimarika ukiangalia katika magoli yake 101 aliyofunga, magoli 49 ameyafunga akiwa ameshafikisha umri wa miaka  30 huku 52 ameyafunga akiwa na umri chini ya miaka 30 maana yake ni kwamba kadri muda unavyokwenda anabaki kuwa bora

Ronaldo pia ni mfungaji bora wa muda wote wa  Uefa Champion league akiwa na mabao  130 huku mshindani wake wa muda wote Lionel Messi akiwa na mabao 115
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad