9/01/2020

Salmin Swaggz Aingilia Bifu la Young Killer na Lunya


Mmoja wa wasanii wanaounda kundi la OMG Tanzania Salmin Swaggz ameliingilia tofauti iliyopo kati ya msanii mwenzake wa kundi hilo Young Lunya na Young Killer kwa kusema paka hawezi kumjibu panya hata siku moja.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Salmin Swaggz amesema kuna watu wa kushindana nao kwenye game, pia huwezi kushindana na kila mtu.

"Kuna watu wakushindana nao kwenye game na sio kila mtu lazima ushindane naye, paka hawezi kudisiwa na panya halafu akajibu lakini ninachomaanisha sio kwamba Young Killer ni paka halafu Young Lunya ni panya hapana ni vitu tofauti, Young Killer alijitengenezea ukubwa wake ila Young Lunya ndiyo wakati wake kwa sasa" ameeleza Salmin Swaggz

Pia amefunguka kuhusu mustakabali wa kundi la OMG kwa kusema halijavunjika na mipango inaendelea japo kila mtu anafanya kazi kivyake ila muda sio mrefu wataachia kazi mpya ambayo itawakutanisha wasanii wote wa kundi hilo ambao ni Young Lunya, Conboi, na Salmin Swaggz
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger