Shuhudia JPM Alivyotandika Pushapu JukwaaniMGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John  Magufuli,  amewaacha hoi wananchi wa Geita baada ya kupanda jukwaani na kuanza kupiga pushapu (push-ups) alipomaliza kuwahutubia katika mkutano wa kampeni zake, leo Jumatano, Septemba 9, 2020.


Magufuli imekuwa kawaida yake kufanya mazoezi hasa ya pushapu kuonyesha ukakamavu wake na utayari wa kuendelea kulitumikia taifa katika wadhifa huo.


Mwaka 2015, katika kampeni zake, Magufuli alikuwa akipiga pushapu katika mikutano yake mingi, jambo ambalo lilimpa umaarufu mkubwa kuwa ni kiongozi shupavu na mwenye nguvu ya kuhimili mikiki-mikiki ya uongozi ambapo mwaka huu ameanza tena kulifanya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments