9/29/2020

T-Bway kuachana na Kim Nana "Madem wameongezeka"

 


T-Bway kuachana na Kim Nana ni moja ya swali ambalo linaulizwa sana kwa watu wa Jamhuri ya mitandao ya kijamii, sasa mtangazaji huyo wa kipindi cha 5Selekt ya East Africa TV amefunguka mwanzo mwisho kuhusu sakata hilo linalondelea kwenye kurasa za habari za kimbea.

Akikata mzizi wa fitna wakati anazungumzia suala hilo kupitia EATV & EA Radio Digital T Bway ameeleza kuwa 

"Sidhani kama nikawa nipo na mtoto halafu mama yake asiwepo au mpaka tupige picha ndiyo mjue kwamba tupo pamoja, kwenye mitandao kuna mambo mengi kuanzia alivyokuwa mjamzito walisema kakimbia mara kajificha hayo mambo yapo ila tupo pamoja yule ni baby mama wangu" amesema T Bway 360.

Wawili hao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Baby Sky, ambapo T Bway amesema tangu amekuwa baba amegundua kuwa madem wamezidi kuongezeka na kumpenda kwa kumuona kama baba bora.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger