9/19/2020

Takwimu zinaiumiza Kagera Sugar dhidi ya Yanga

Klabu ya Kagera Sugar itakua mwenyeji wa Yanga hii leo katika muendelezo wa michuano ya Ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo imeingia katika raundi yake ya tatu.


Kagera inayonolewa na Kocha Mecky mexime,inausaka ushindi wake wa kwanza msimu huu kufuatia kupoteza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya JKT Tanzania kwa bao 1-0 na kutoka suluhu ugenini dhidi ya Gwambina.


Yanga wao watakua wakihitaji ushindi wa pili mfululizo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons.


Msimu uliopita, Kagera iliiadabisha Yanga katika Uwanja wa Mkapa kwa kuwalaza bao 3-0 lakini Yanga walijibu kiasi kwa kushinda Kaitaba kwa bao 1-0.


Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba,East Africa Radio inakusogezea takwimu za mechi tano za mwisho baina ya miamba hiyo miwili ya soka ilipokutana katika Uwanja wa Kaitaba.


2015/16-Kagera 0-2 Yanga


2016/17- Kagera 0-2 Yanga


2017/18-Kagera 2-6 Yanga


2018/19-Kagera1-2 Yanga


2019/20-Kagera 0-1 Yanga


Yanga Sc haijapoteza mchezo wowote katika mechi tano za mwisho dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger