9/24/2020

Umoja wa Ulaya wasema Lukashenko sio rais halali wa BelarusUmoja wa Ulaya umesema hii leo kwamba rais Alexander Lukashenko sio kiongozi halali wa Belarus. Umoja huo umesema hatua ya kuapishwa haraka Lukashenko kuingia madarakani ni kitendo kilichokwenda kinyume na matakwa ya wananchi wa Belarus.

Taarifa ya pamoja ya nchi zote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya iliyotolewa imebaini kwamba kile kilichoitwa kuapishwa madarakani, na mamlaka mampya yanayodaiwa na Lukashenko yanakosa uhalali wa kidemokrasia wa aina yoyote. 


Taarifa hiyo imekwenda mbali zaidi na kusema kwamba kuapishwa huko kwa Lukashenko kunakwenda kinyume na matakwa ya sehemu kubwa ya idadi ya watu wa Belarus kama ambavyo imejionesha kupitia maandamano makubwa ya umma nchini humo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger