10/27/2020

Billnass Afunguka Ukweli Mchungu "Nandy Anaingiza Hela zaidi Yangu"

 


Billnass aanika wazi kwamba Nandy anaingiza pesa nyingi zaidi yake. Kwenye mahojiano na kipindi cha Leo Tena Clouds FM, Nenga amesema Nandy anapata shoo nyingi na pia ana miradi mingi zaidi yake.


Akijibu swali la nani kati yao anaingiza fedha zaidi, Billnass alijibu kuwa ni Nandy lakini akaenda mbali na kufafanua kuwa yeye ndio mwenye fedha nyingi zaidi ya Nandy kutokana na matumizi ya mchumba wake huyo.

 

“Nandy anaingiza pesa zaidi yangu, anapata shoo nyingi na ana miradi mingi. Lakini mwisho wa siku tukiwa tunafanya tathimini za nani ana pesa nyingi kwenye akaunti, mimi ndio nakuwa juu,” amesema billnass na kuongeza

 

“Hiyo inatokana na kuwa Nandy ana matumizi mengi kuliko mimi, kwa hiyo huingiza pesa nyingi lakini pia hutumia pesa nyingi zaidi.” alimaliza Billnass ambaye safari hii ameshirikishwa na Nandy kwenye 'Do Me' wimbo wao mpya unaofanya vizuri kwa sasa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger