10/27/2020

Wanajeshi wawili, wapiganaji 21 wauawa katika makabiliano DR Congo

 


Wanajeshi wawili na wapiganaji 21 wameuawa katika kipindi cha siku tatu za makabiliano katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

Jeshi la serikali limesema lilizindua operesheni iliyoanza Ijumaa baada ya kutokea mashambulizi kadhaa kutoka kwa kundi la waasi wa CODECO.


 Luteni Jenerali Philemon Yav amesema wanajeshi wawili waliuawa na wengine wanne wakajeruhiwa katika eneo la Walendu Tatsi, mashariki mwa mji mkuu wa mkoa wa Ituri, Bunia. 


Amesema eneo hilo lipo chini ya udhibiti wa vikodi vya serikali baada ya makabiliano hayo yaliyoendelea hadi Jumapili, na kulazimisha idadi kubwa ya wakaazi kukimbilia usalama wao mwishoni mwa wiki. 


Waasi wa CODECO walikubali kusitisha mashambulizi dhidi ya wapinzani wao wa kikabila baada ya Rais Felix Tshisekedi kulituma Ituri kundi la wababe wa zamani wa kivita mwezi Agosti. Kundi hilo la kisiasa na kidini linatuhumiwa kwa mauaji ya mamia ya raia tangu Desemba 2017.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger