Fahamu, kutokupumzika kunavyoathiri afya ya akili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Msaikolijia kutoka Chama cha Wanasaikolojia Tanzania, Neema Kessy, amesema kukosa kupata muda wa kupumzika kuna changia katika kuzorotesha afya ya akili.

 

Akizungumza katika kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Neema, amesema kuwa kupata muda mzuri wa kupumzika kuna changia katika  kuboresha afya ya akili.


“Kutokupata muda mzuri wakupumzika limekuwa tatizo kwa watu wengi sana, tunapumzika kidogo kwasababu mbalimbali ambazo tunazipata kwa ajili ya kusaka kipato, tunatakiwa tuhakikishe tunapata muda wa kutosha wa kupumzika huo utatufanya afya yetu ya akili ikae vizuri” amesema Neema Kessy


Aidha Msaikolojia huyo ameitaja michezo kuwa mmoja ya kigezo kinachosaidia kustawisha si tu afya ya mwili bali na akili pia, “Kufanya mazoezi itakusaidia kufanya afya ako ya mwili iwe vizuri lakini na afya ya akili nakukuondelea yale magonjwa yasiyoambukiza ambayo watu wengi walioingia kwenye magonjwa yasiyoambukiza yameathiri afya yao ya akili" amesema Neema Kessy

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad