Hii Lazima Inakuhusu....Walaji wa Chapati, maini na SODA Wapewa Angalizo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mtaalam wa masuala ya lishe kutoka Jukwaa la lishe Tanzania (PANITA) Jane Msagati, amewashauri wanaopenda kula chapati na maini na kisha wakashushia soda au chai ya rangi, waache ulaji wa mtindo huo na badala yake washushie juice ya matunda ili kusaidia mwili kuzalisha damu ya kutosha.

 

Ushauri huo ameutoa hii leo Oktoba 24, 2020, wakati akizungumzxa kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio  na kusema kuwa mtu anapokula hivyo unauwekea uzito mwili wake kuwa na uwezo wa kufyonza virutubishi.


"Mara nyingi tuepuke kula vyakula vyenye viurutubishi vya madini chuma ambavyo vinasaidia katika uzalishaji wa damu mwilini na vitu kama soda na chai ambavyo mara nyingi huzuia ufyonzaji wa virutubishi katika mwilini, hali inayopelekea miili yetu kuwa na upungufu wa hivyo virutubishi", amesema Jane.


Aidha ameongeza kuwa, "Mtu anapokula chapati na maini, ashushie na juice iliyotengenezwa na matunda na maji yaliyo salama kwa sababu matunda ni vyanzo vizuri vya vitamin C, unausaidia sana mwili kuzalisha damu ya kutosha kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya mwili wa mwanadamu".


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad