10/09/2020

Jeshi la Polisi latoa maelekezo kuhusu ukatili

  


Wakati Dunia ikielekea kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Oktoba 11, 2020 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia Dawati la Jinsia na Watoto limesema jamii izingatie kukomesha mila na desturi ambazo bado zimekuwa zikiripotiwa kuwa chanzo cha kusababisha ukatili wa kijinsia.

 

Katika maadhimisho hayo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Leah Mbunda amesema bado kuna vitendo vingi vya kinyanyasaji hususani kwa mtoto wa kike na mara nyingi kesi hizo zimekuwa zikitendwa hasa na watu wa karibu zaidi na watoto hawa pasipo kuzingatia athari za baadaye.


Kwa upande wao washiriki wamesema ili jamii izidi kuwaamini baadhi ya mabinti waliopata nafasi za uongozi kwenye serikali na taasisi mbalimbali hawana budi kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi, huku wengine wakishauri kuwepo kwa mafunzo endelevu kwa mtoto wa kike ili kumjengea uwezo pamoja wadau kuachilia fikira za mfumo dume ambao umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu.


Kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ni "Tumwezeshe Mtoto wa Kike; Kujenga Taifa Lenye Usawa"


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger