10/02/2020

Joh Makini amuweka kando mdogo wake Nikki wa Pili

Msanii wa HipHop Joh Makini amewataja wasanii kama Lord Eyes, G Nako Warawara na Fid Q kama ndiyo wasanii pekee ambao wapo katika kizazi chake cha marapa wakali Bongo huku akimtoa mdogo wake Nikki wa Pili kwa kusema ana era yake tofauti.


Joh Makini amesema hayo kwenye kipindi cha SalamaNa ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku ambapo alikuwa anawataja wasanii wa HipHop ambao anawakubali.


 "Kwenye kizazi changu mimi kuna marapa wakali wengi tu kama Lord Eyes, Gnako na FidQ lakini Nikki wa Pili simuweki hapa, yeye ana 'era' yake pia" amesema Joh Makini 

"Mimi na Lord Eyes tumetoka mbali tangu mihangaiko ya Arusha hadi kuja Dar na kukaa pamoja, hali yake ambayo aliipitia wote ilituhuzunisha lakini na hatukuwa na chakufanya  ulikuwa wakati mgumu kwetu" ameongeza 


Joh Makini, Lord Eyes, Nikki wa Pili na G Nako ni wasanii wa HipHop ambao kwa pamoja wanatokea kwenye kampuni ya Weusi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger