10/27/2020

Kamanda Muroto “Polisi Tumewezeshwa Kufanya Doria”

 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto amesema kuwa kuelekea uchaguzi mkuu usalama wa raia na mali zao umeimarishwa katika mkoa huo.


Muroto amesema hayo muda mfupi uliopita jijini Dodoma na kusema kuwa katika kufanikisha jambo hilo Jeshi la Polisi mkoani humo litashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kama Jeshi la Magereza,Mgambo ,Uhamiaji na Zimamoto.


“Tayari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge ametuwezesha usafiri kwa ajili ya kufanya doria na kusafirisha vifaa mbalimbali vitakavyotumika kwenye uchaguzi huo kutoka sehemu moja kwenda nyingine ” Kamanda Muroto.


Aidha, Kamanda Muroto amesema kuwa kutakuwa na askari kwa kila kituo kidogo cha kupigia kura ambao wote kwa pamoja watakutana sehemu kuu ya majumuisho ili kuhakikisha usalama wa sehemu husika unaimarika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger