Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kenny afunguka kuhusu Alikiba na Harmonize

 


Muongozaji wa video hapa nchini Director Kenny amesema hana noma na msanii Alikiba na Harmonize kwenye suala zima la kutaka kufanya nao kazi japo stori zinadai sehemu anayofanyia kazi 'production' inambana asifanye kazi na wasanii hao.

 

Akizungumza kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio Director Kenny ameeleza kuwa kikubwa ni makubaliano ya bajeti endapo akifanya kazi na wasanii hao pia kazi atakayoifanya ifike mbali.


"Hii ni Production ambayo ina deal na msanii yeyote kwa atakayefika kiasi ambacho kinapatikana kwa sababu kadri siku zinavyozidi kwenda ndiyo tunatakiwa kufanya vitu vikali zaidi, sijabanwa kwamba nisifanye video na mtu fulani ila ni bajeti ya mtu tu" amesema Director Kenny 


"Mimi sina noma na Alikiba wala Harmonize ninachotaka ni tufanye kazi iende mbali hiyo ndiyo future yangu, zamani niliwahi kumcheki Ali ili tufanye kazi ilikuwa kipindi cha mwaka 2016 au 2015" ameongeza

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments