10/07/2020

Kiba Amkataa Mrembo wa MondiDAR: Siku chache tangu video queen wa nchini Rwanda, Mbabazi Shadia ‘Shaddy Boo’ aposti video inayoonesha gari aina ya Range Rover likiwa na ‘pleti namba’ yenye jina la mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na kuzua gumzo kama lote mitandaoni, hatimaye jamaa ameibuka na kumkataa laivu mrembo huyo.


Kitendo cha mrembo huyo kuposti tu picha hiyo, watu walijiongeza kwa kusema kuwa, huwenda mrembo huyo ambaye iliwahi kutajwa kuwa ndiye atakayeolewa na kinara mwingine wa Bongo Flea, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ana uhusiano na King Kiba.

Gumzo sasa likaenda mbali zaidi kwa watu kusema mitandaoni kuwa, Kiba ameingia kwenye anga za Diamond au Mondi kwani tayari ilisharipotiwa kuwa, mrembo huyo ndiye atakayeziba pengo la Tanasha Donna aliyekuwa mwandani wa Mondi kabla ya kutengana mapema mwaka huu.


KIBA AFUNGUKA


Baada ya mambo kuwa mengi, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Kiba na kufanikiwa kufanya naye mahojiano ambapo alikiri kumfahamu mrembo huyo, lakini akasema hakuna cha zaidi kati yao.


IJUMAA: Mambo Kiba?


KIBA: Poa tu.


IJUMAA: Kiba tunataka kujua, uhusiano wako na mrembo Shaddy Boo kutoka nchini Rwanda ukoje ni wa kikazi au vipi?


KIBA: Hatuna uhusiano wowote kikazi, kifamilia na wala ki-personal (kibinafsi); yaani kiufupi hatuongeagi chochote.


IJUMAA: Ina maana humfahamu kabisa?


KIBA: Kumfahamu, ninamfahamu kuwa ni msichana ambaye anakaa Rwanda, ni socialite (mrembo maarufu mtandaoni).


IJUMAA: Juzikati aliposti video ikionesha gari kwenye akaunti yake huku plate number zikiwa na jina lako, hili unalizungumziaje?


KIBA: Sina cha kusema kwa sababu nimeshaeleza kila kitu kuwa sina ukaribu wowote na huyo dada zaidi ya kumfahamu tu kuwa ni mrembo kutoka Rwanda, kama alifanya hivyo, siyo mbaya, pengine ni mapenzi tu ya kishabiki aliyonayo kwangu.


TUJIKUMBUSHE


Miezi michache iliyopita kulikuwa na tetesi kibao mitandaoni kuwa Kiba ameachana na mkewe Amina Khaleef huku chanzo cha kuachana kwao kikiwa hakijulikani.

Lakini baada ya muda mrefu kupita wawili hao walionekana tena pamoja huku wakioneshana mahaba kama yote, jambo lililoleta minong’ono mingi kwa baadhi ya mashabiki.

Hatujakaa sawa wakati Kiba na mkewe wakiendelea kula bata, ghafla mrembo Shaddy Boo kutoka nchini Rwanda akaposti video kwenye Insta Story yake ikionesha gari aina ya Range Rover nyeupe huku ikiwa na plate number yenye jina la King Kiba, jambo lililoibua sintofahamu kwa mashabiki.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger